Enrolment options

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KOLEJI YA SANAA NA SAYANSI ZA JAMII IDARA YA LUGHA NA TAALUMA ZA FASIHI FASIHI LINGANISHI Madhumuni ya Kozi Kozi hii ina lengo la kumwezesha mwanafunzi kupata mwanga wa jumla kuhusu dhana ya mwingiliano wa Fasihi za jamii mbalimbali za hapa Ulimwenguni. Kwa namna moja au nyingine, mwingiliano huo husaidia kuleta umoja katika uga wa Fasihi. Maelezo ya Kozi: Kozi hii ni ya semesta moja na ina vigezi vitatu. Ni kozi ambayo inapanua upeo wa mwanafunzi katika kulinganisha vipengele mbalimbali vya Fasihi ya Kiswahili na Fasihi za jamii nyingine hapa duniani kama vile Fasihi ya Ulaya, Fasihi ya Kichina, Fasihi ya Kijapani, Fasihi ya Mashariki ya Kati na Fasihi ya Kiafrika. MADA: 1. Usuli wa Fasihi 1.1 Dhana ya Fasihi 1.1.1 Maana na asili 1.1.2 Dhima ya Fasihi katika jamii 1.1.3 Tanzu za Fasihi 1.1.4 Mitindo ya Fasihi 1.1.5 Nadharia za Fasihi 1.2 Dhana ya Ujumi katika Fasihi 1.2.1 Maana na asili ya Ujumi 1.2.2 Mdhihiriko wa Ujumi katika kazi za Fasihi 2. Dhana ya Fasihi Linganishi 2.1 Fasili yake 2.2 Sifa za Mwana Fasihi Linganishi 2.3 Chimbuko na Mikondo Mikuu ya Fasihi Linganishi 2.4 Dhana muhimu katika taaluma ya Fasihi Linganishi 2.4.1 Fasihi ya Kiswahili na/au fasihi ya kitaifa 2.4.2 Fasihi ya kitaifa na fasihi ya kimataifa/ya kiulimwengu 2.5 Umuhimu wa taaluma ya Fasihi linganishi 2.6 Misingi ya Fasihi Linganishi 2.7 Matatizo ya Fasihi Linganishi 3. Vipengele vya ulinganisho 3.1 Fani (Muundo, wahusika, mandhari n.k) 3.2 Maudhui (dhamira zinazojichomoza) 3.3 Utamaduni 3.4 Itikadi 3.5 Historia 4. Uhakiki linganishi 4.1 Riwaya ya Kiswahili na riwaya ya jamii nyingine 4.2 Tamthiliya ya Kiswahili na tamthiliya ya jamii nyingine 4.3 Ushairi wa Kiswahili na ushairi wa jamii nyingine 5. Hadhi ya Fasihi ya Kiswahili katika Fasihi ya Ki-ulimwengu vii Ufundishaji: Saa 45 (Mihadhara 30 na Semina 15) Tathmini: Tamrini 40% (semina 5%, k/kundi [utafiti wa maktabani] 10%, jaribio 25%) na Mtihani wa Mwisho 60%. Marelejeo Aldridge, A.O. (1969). Comparative Literature: Matter and Method. Urbana. University of Illinois Press Sheriff, I. (1988) Tungo Zetu. Trenton.the Red Sea Press Bentocini, E. (1989), Outline of the Swahili Literature. Leiden. E.J. Brill Knappert, J. (1979), Four Centuries of Swahili Verse. London. Heinemman Posnett, H.M. (1970), Comparative Literature. New York. Johnson Stallknecht, N.P. and Horst Frenz (1961), Comparative Literature: Method and Perspective, Southern IllinoisUniversity Press, CARBONDALE Totosy, S.Z. (1998), Comparative Literature: Theory, Method, Application, GA, Amsterdam. Weisstein, U. (1973), Comparative Literature and Literary Theory: Survey and Introduction. Bloomington and London. Indiana University PreSS

Guests cannot access this course. Please log in.